Skip to main content

Idadi ya watafuta hifadhi yaongezeka kwenye mataifa yaliyostawi

Idadi ya watafuta hifadhi yaongezeka kwenye mataifa yaliyostawi

Ripoti kutoka kwa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR inasema kuwa idadi ya watafuta hifadhi kwenye mataifa yaliyostawi iliongezeka kwa asilimia 20 mwaka 2011 hali iliyochangiwa na mizozo kwenye nchi za kiarabu na kaskazini mwa Afrika.

Jumla la watafuta hifadhi 441,000 waliandikishwa mwaka uliopita tofauti na watu 368,000 walioandikishwa mwaka 2010 kwenye  mataifa 44 yaliyostawi.

Ripoti hiyo kutoka mataifa 44 kutoka Ulaya, Marekani, Australia na maeneo ya bara Asia inasema kuwa ongezeko kubwa lilishuhudiwa kusini mwa Ulaya ambapo watafuta hifadhi waliongezeka mara mbili zaidi.

Tariq Abu Shabaki kutoka UNHCR anasema kuwa ni nchi za kaskazini mwa Ulaya na pia zile zilizo kaskazini mwa bahari ya Atlantic na Australia zilishuhudia kupungua kwa idadi ya watafuta hifadhi.

(SAUTI YA TARIQ ABU SHABAKI)