Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kofia ya Samawati ni ishara ya amani:Ban

Kofia ya Samawati ni ishara ya amani:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa kofia ya Samawati ni ishara ya matumaini.

Akitoa hotuba kuhusu changamoto za kulinda amani nchini Indonesia Ban amesema kuwa  ameajionea jinsi walinda amani wanavyoleta mabadiliko kwa maisha ya watu.

Ban amesema kuwa wakati kuna mizozo wanafunzi  hukosa kwenda shuleni  hadi wakati walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanapoingilia kati na kutuliza hali ili watoto waende shuleni.

Ameongeza kuwa walinda amani huwa wanajenga madaraja yakiwemo ya kupitia  na madaraja ya uaminifu kati ya jamii.

Pia huondoa mabomu ya ardhini ili wakulima wapate kuendelea na shughuli zao.