Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi ya mabomu nchini Syria

Ban alaani mashambulizi ya mabomu nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekashifu vikali mashambulizi ya mabomu yaliyotekelezwa kwenye mji mkuu wa Syria Damascus mwishoni mwa juma ambapo watu kadhaa waliuawa na wengi kujeruhiwa.

Ban pia alituma rambi rambi zake kwa jamaa za waathiriwa na kwa watu wa Syria na kutaka kusitishwa kwa ghasia nchini humo. Ripoti za vyombo vya habari zinaeleza kuwa takriban watu 27 waliuawa na wengine 100 kujeruhiwa baada ya kile kilichotajwa kuwa mabomu yaliyokuwa kwenye gari kulipuka. Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa ni kuwa zaidi ya watu 8000 wengi wakiwa ni raia wameuawa na maelefu ya engine wakilazimika kuhama makwao tangu kuanza kwa mzozo nchini humo.