Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa fedha watishia oparesheni ya kuhamisha wahamiaji Yemen

Ukosefu wa fedha watishia oparesheni ya kuhamisha wahamiaji Yemen

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM mwezi huu linatarajiwa kuongoza oparesheni ya mwisho ya kusafirisha wahamiaji 277 wa Ethiopia waliokwama nchini Yemen ikiwa ufadhili mpya hautatolewa.

Hadi sasa IOM imesaidia zaidi ya wahamiaji 6000 raia wa Ethiopia kurejea nyumbani kutoka mji wa Haradh ulio karibu na mpaka ambao umekuwa ukitumiwa na wahamiaji  kama kituo cha kuingia nchini Saudi Arabia.

Hali ya kimaisha kwa wahamiaji kwenye mji huo imatajwa na wafanyikazi wa IOM kuwa mbaya zaidi na inayozidi kuwa mbaya kutokana na kuendelea kuongezeka wahamiaji zaidi huku kukiwa na misukosuko kati ya wahamiaji na wenyeji.

Juma lilipota gazeti moja lilichapisha picha za wahamiaji waliokatwa viungo vya mwili na kundika ripoti za wahamiaji waliotekwa na wanaolazimishwa na watekaji wao kuitisha fidia kutoka kwa familia zao.