Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yahofia hatma ya watoto waliokumbwa na ghasia Gaza na Israel

UNICEF yahofia hatma ya watoto waliokumbwa na ghasia Gaza na Israel

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeelezea hofu yake kuhusu hatma ya watoto kufuatia ghasia za hivi majuzi kwenye Ukanda wa Gaza na nchini Israel. Jana Jumatatu kijana wa Kipalestina wa umri wa miaka 15 aliuawa na wengine wanne kujeruhiwa kufuatia mlipiko uliotokea kwenye ukanda wa Gaza.

Hadi sasa watoto 14 wa kipalestina walio umri wa kati ya mwaka mmoja na miaka 17 wanaripotiwa kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya angani huku shule mbili zikiharibiwa. Sijku ya Jupapili kombora lilinguka kwenye shule moja ambayo haukuwa na wanafunzi nchini Israel hali iliyopelekea kusitishwa kwa masomo kusini mwa nchi. Mjumbe maalum wa shirika la UNICEF kwenye sehemu iliyokaliwa ya kipalestina Jean Gough anasema kwamba kila jitihada zinahitajika kufanywa kulinda watoto wasiokuwa na hatia.