Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majaji wapya wa mahakama ya ICC waapishwa

Majaji wapya wa mahakama ya ICC waapishwa

Majaji wapya watano waliochaguliwa hivi karibuni kwa ajili ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC wameapishwa. Majaji hao walichaguliwa mapema mwezi wa disemba mwaka jana waliapishwa mwishoni mwa wiki na kufuatiwa na tafrija fupi.

Walioapishwa ni pamoja na Howard Morrison kutoka Uingereza, Anthony T. Carmona wa Trinidad and Tobago, Olga Herrera Carbuccia anayetoka Jamhuri ya Dominican. Wengine ni Robert Fremr wa Jamhuri ya Czech, Eboe-Osuji kutoka Nigeria, Wote kwa pamoja wanatazamia kutumikia mahakama hiyo yenye makao yake The Hague kwa kipindi cha miaka nane.