Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Quartet yapongeza juhudi za Jordan katika kusaka amani mashariki ya kati

Quartet yapongeza juhudi za Jordan katika kusaka amani mashariki ya kati

Mpango wa kimataifa wa pande nne wenye lengo la kutafuta amani ya kudumu Mashariki ya Kati yaani Quartet unaojumuisha Umoja wa Mataifa, Urusi, Marekani na Muungano wa Ulaya, wamekutana Jumatatu kutathimini maendeleo yaliyopatikana tangu walipotoa taarifa yao Septemba mwaka 20011.

Quartet inasema kimsingi bado inazingatia malengo waliyoyaweka katika taarifa yao ya mwaka jana na hivyo wanakaribisha juhudi muhimu zilizofanywa na serikali ya Jordan tangu mwezi Januari mwaka huu kama sehemu ya kushirikiana majukumu ili kufikia muafaka ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Quartet pia imejadili hali mbaya inayoendelea Gaza na Kusini mwa Israel wakielezea hofu yao juu ya machafuko yanayoendelea na kutoa wito kwa pande zote kujizuia na kurejesha hali ya utulivu.

Mpango huo wa pande nne pia umezitaka pande zote kuendelea kutimiza wajibu wao na kujiepusha na hatua zozote  zitakazochochea ghasia.

Mpango huo sasa utakutana tena mjini Wanshington mwezi ujao wa April.