Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwekeza kwa wanawake wa vijijini ni uwekezaji mwerevu : Ban

Kuwekeza kwa wanawake wa vijijini ni uwekezaji mwerevu : Ban

 

Leo ni siku ya kimataifa ya wanawake na kauli mbiu ya mwaka huu ni kuwawezesha wanawake wa vijijini.

Wanawake wa vijijini wanaweza kuboresha maisha ya jamii nzima endapo watapewa fursa ya kuwa na rasilimali na kutobaguliwa.

Hiyo ni kauli iliyosemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake ambayo kila mwaka husherehekewa Machi 8.

Ban amesema kuwekeza katika wanawake wa vijijini ni uwekezaji mwerevu katika maendeleo ya mataifa duniani.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban ameongeza kuwa ni suala lisilokubalika kuona kwamba wanawake wakulima ambao ndio wazalishaji wakubwa wanapata asilimia 5 pekee ya msaada wa kilimo.