Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazindua kuhusu fursa ya ICT kwa wanafunzi wenye ulemavu

UNESCO yazindua kuhusu fursa ya ICT kwa wanafunzi wenye ulemavu

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na kampuni ya Microsoft wamezindua ripoti kuhusu fursa ya teknolojia ya mawasiliano yaani ICT na uwezo wa kujifunza kwa wanafunzi wenye ulemavu.

Uzinduzi huo umefanyika kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu teknolojia saidizi na watu wenye ulemavu unaofanyika mjini San Diego hapa Marekani.

Mafunzo maalumu kwa wenye ulemavu yanahitaji kuzingatia mahitaji binafsi kwa wanafunzi wote na kutambua kwamba wana mifumo tofauti ya kujifunza ikiwemo wanafunzi wenye ulemavu kiasi na wenye ulemavu mkubwa.

 UNESCO inasema teknolojia inachukua jukumu muhimu katika kuandaa muhula wa masomo na kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu kushiriki sawia na wasio na ulemavu katika kujifunza.