Ban amtaka msaidizi wake kutembelea Syria kuangalia hali ya misaada ya kibinadamu

23 Februari 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemwomba mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa kutembelea nchini Syria ili kufanya tathmini namna huduma za kibinadamu kwenye eneo hilo, ambalo linashuhudiwa vikosi vya serikali vikiendelea kuyaandama makundi ya waandamanaji.

Ban amemwomba Bi Valerie Amos kwenda nchini humo ili hatimaye kubainisha namna mahitajio ya kimisaada ya kibinadamu yalivyo na wakati huo huo kuweka msukumo mpya juu ya kuheshimiwa kwa matakwa ya kidemokrasia.

Kwa m ara kadhaa maafisa wa Umoja wa Mataifa wamepaza sauti dhidi ya utawala wa kimabavu wa kisitisha matumizi ya kijeshi kuwaandama waandamanaji wa kiraia wanaotaka mabadiliko kwenye mfumo wa uongozi.

Mamia kadhaa ya watu wamepoteza maisha tangu kuanza kwa vuguvugu la maandamano ya amani yanayopinga utawala wa Assad .

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter