Baraza la Usalama laipongeza Yemen kwa kuendesha uchaguzi katika hali ya amani

23 Februari 2012

Baraza la usalama limekaribisha hatua ya kufanyika kwa uchaguzi nchini Yemen na limewahimiza vingozi wa kisiasa nchini humo kutorudi nyuma hasa wakati huu kukiwekwa misingi mipya ya kuimarisha demokrasia ya taifa hilo ambalo hivi karibuni lilitumbukia kwenye machafuko ya kiraia.

Baraza hilo la usalama limewapongeza wananchi wa Yeme kwa utulivu na usikifu na hatimaye kufanikisha uchaguzi na limetaka ushiriki wa pamoja toka makundi yote

Limeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zote za ujenzi mpya wa mifumo ya kidemokrasia na likazitaka mamlaka zilizopo kutelekeza kwa vitendo maazimio yanayotaka maridhiano ya pande zote.

Ama kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza pia wananchi wa Yemen ikiwemo pia makundi ya vijana ambao anaarifiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter