Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na taasisi ya kimataifa ya amani watia saini makubaliano

UNESCO na taasisi ya kimataifa ya amani watia saini makubaliano

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova amesisitiza kuali ya wahenga kwamba Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Akizungumza katika hafla maalumu ya kusaini makubaliano baina ya UNESCO na taasisi ya kimataifa ya amani iliyoanzishwa na balozi mwema wa UNESCO na mcheza filamu maarufu Forest Whitaker, chuo kikuu cha Rutgers New Jersey hapa Marekani na serikali ya Marekani, amesema mtu akiwa peke yake anaweza kuleta mabadiliko lakini wakiwa wengi wanaweza kubadili dunia.

Maafikiano hayo yanakifanya chuo kikuu cha Rutgers kuwa ndio chuo kikuu pekee cha elimu ya juu kwa ushirika rasmi wa UNESCO. Ushirika huo unatoa fursa adimu ya kushughulikia masuala ya amani na kupinga ghasia katika ngazi ya kimataifa.

Forest Whitaker amesema anatumai kwamba taasisi hiyo itafungua njia ya majadailiano ya kupatikana kwa amani ya kudumu, sio tuu kupitia kazi za watunga sera bali pia jamii. Ameongeza kwa watakuwa na miradi kama hiyo pia Afrika akizitaja nchi za Sudan Kusini na Uganda ambazo zimeorodheshwa katika mpango huo.