Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana duniani watiwa hofu na ukosefu wa ajira

Vijana duniani watiwa hofu na ukosefu wa ajira

 

Vijana kote duniani wanatiwa hofu kutokana na ukosefu wa fursa za ajira na wanatoa wito wa kuongezwa uwekezaji katika eneo hilo la ajira . Hii ni kutokana na ripoti mpya ya kimataifa ya vijana iliyotolewa Jumatatu na Umoja wa Mataifa.

Baada ya matatizo ya uchumi yanayoendelea kuighubika dunia tatizo la ajira kwa vijana duniani limeongezeka mara dufu na kuvunja rekodi mwaka 2009 ambapo watu milioni 75.8 wasio na ajira ni vijana. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumzia hali hiyo amesema leo hii dunia ina idadi kubwa ya vijana kuliko wakati mwingine wowote, na wanadai haki zao, na kuwa na sauti katika masuala ya uchumi na siasa. Alice Kariuki anaripoti.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)