Viongozi wa Afrika wahudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 40 ya shirika la UNEP

Viongozi wa Afrika wahudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 40 ya shirika la UNEP

Viongozi wa zaidi ya mataifa 30 wameshiriki kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 40 ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP zilizofanyika wakati wa mkutano wa 18 wa Muungano wa nchi za Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Sherehe hizo ziliongozwa na rais wa Kenya Mwai Kibaki aliyeungana na marais wengine 33 na serikali akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, mwenyekiti wa Muungano wa Afrika Jean Ping pamoja mkurugenzi wa UNEP Achim Steiner.

Ban alimshukuru rais Kibaki kwa kuandaa sherehe hizo na kuwashukuru pia wananchi wa Kenya kwa kutoa makao ya shirika hilo yaliyo mjini Nairobi tangu mwaka 1972.