Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi waombwa kutilia maanani masuala ya kuwafaidi watu

Viongozi waombwa kutilia maanani masuala ya kuwafaidi watu

Kamati kuhusu maendeleo ya dunia imesema kuwa viongozi wanastahili kutilia maanani masuala muhimu yanayowafaidi watu. Kamati hiyo iliyobuniwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon mwaka 2010 ili kutoa mwelekeo kuhusu maendeleo endelevu na inaongozwa na mwenyekiti mwenza rais wa Finland Tarja Halonen pamoja na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. 

Akizungumza kwa njia ya video mwenyekiti mwenza wa mkutano Halonen amesisitiza umuhimu wa kuwaweka watu kuwa kitovu cha kufikia maendeleo endelevu, kutokomeza umasikini na kuimarisha usawa na ni lazima vipewe kipaumbele na jumuiya ya kimataifa. Jopo hilo limesema kuwawezesha wanawake na kuwahakikishia jukumu kubwa katika masuala ya uchumi ni muhimu sana katika maendeleo endelevu. 

Katibu Mkuu akipokea ripoti ya jopo hilo amesema maendeleo endelevu ni suala lililo katika ajenda ya juu ya muhula wake wa pili. 

(SAUTI YA BAN KI-MOON) 

Katibu Mkuu amewashukuru wenyeviti wenza Halonen na Zuma na wjumbe wote kwa mchango wao na kuzitaka sekta zote za jamii kujiungakatika juhudi hizo za maendeleo. 

Ripoti ya jopo hilo ni mchango mkubwa katika kazi ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo na inachangia katika maandalizi ya mkutano wa Rio+20 utakaofanyika June 2012 Brazil. Wajumbe 22 wa jopo hilo wanajumuisha wakuu wan chi wa sasa na wa zamani, mawaziri na wawakilishi wa sekta binafsi na jumuiya za kijamii.