Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka nchi za Afrika kuruhusu haki ya kiuchumi na kisiasa

Ban ataka nchi za Afrika kuruhusu haki ya kiuchumi na kisiasa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-mooon amezitaka nchi za kiafrika kuruhusu haki za kiasiasa, kiuchumi kijamii na kitamaduni ili kuchangia katika kuleta udhabiti na maendeleo kwenye bara la Afrika.

Akihutubia viongozi wa bara la Afrika waliokusanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa muungano wa Afrika Ban ametaja ubaguzi wa kijinsia kama moja ya masuala ambayo yamepuuzwa na nchi nyingi. Ban pia amezitaka nchi za kiafrika ambazo zitaandaa uchaguzi wa urais na Ubunge mwaka huu kuhakikisha kuwa umefanyika kwa njia ya amani.