Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu la UM akutana na mwenzio wa Baraza la Usalama

Rais wa Baraza Kuu la UM akutana na mwenzio wa Baraza la Usalama

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amekuwa na majadiliano na mwakilishi wa Afrika Kusini ambaye kwa sasa anashikilia urais wa mzunguko wa Baraza la Usalama ambako wamejadilia masuala kadhaa.

Miongoni mwa mada zilizopewa uzito kwenye majadiliano hayo, viongozi hao wamegusia pia hoja ya hivi karibuni juu ya uanzishwaji wa mashirikiano ya karibu baina ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Hawakuweka kando meeneo mengine ikiwemo hali ya mambo huko Somalia,Yemeni, Sudan ambako kunashuhudiwa hali ya mkwamo wa kisiasa na kukosekana kwa utengamao wa amani.

Wamezungumzia pia masuala ya kiuchumi na kugusia kwa kina juu ya mkwamo wa hali ya uchumi wa dunia.

Kuhusu hali jumla ya huko Mashariki ya kati, wote kwa pamoja waliweka uzito wa pekee hasa wakati huu ambako pande zote mbili zinazozozana zikiarifu utayari wao wa kurejea kwenye mazungumzo ya moja kwa moja.