Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango ya fedha ya muda mfupi ni kikwazo cha mabadiliko ya biashara:UNEP

Mipango ya fedha ya muda mfupi ni kikwazo cha mabadiliko ya biashara:UNEP

Utafiti uliofanywa karibuni na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP umebaini kuwa mipango ya fedha ya muda mfupi ni kikwazo kikubwa katika mabadiliko ya biashara.

Utafiti huo uliofanyika katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali umeonyesha kwamba asilimia 88 ya wataalamu 642 waliohojiwa wanaona kuna shinikizo kwa matokeo ya mipango ya muda mfupi ya fedha katika kuzifanya biashara kuwa endelevu.

Utafiti huo uliofanyika mwezi Desemba mwaka 2011 uliwauliza wataalamu endapo wanadhani kuna sababu kadhaa ambazo ni vikwazo vya biashara endelevu na mipango ya fedha ya muda mfupi ilitajwa na walio wengi. Sababu nyingine kubwa iliotajwa ni kutokuwepo muafaka wa kanuni na uelewa mdogo wa biashara. Pia mahitaji hafifu ya wateja, ukosefu wa nyezo za kufanyia kazi kwa viongozi na upungufu katika viwango vya kimataifa.