Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuchunguza madai ya dhuluma kwa watoto nchini Haiti

UM kuchunguza madai ya dhuluma kwa watoto nchini Haiti

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa unachunguza kesi za dhuluma za kingono zinazotajwa kutekelezwa kwa watoto na wanajeshi wake nchini Haiti. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema kuwa Kesi ya kwanza inahusu maafisa wa polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL kwenye mji mkuu Port-au-Prince huku kesi ya pili ikiwa inahusu maafisa wa kikosi cha polisi kilichobuniwa cha FPU kwenye mji wa Gonaives.

Ujumbe wa Umoja wa Mataiafa nchini Haiti MINUSTAH unasema kuwa uchunguzi ulianza punde tu madai hayo yalipotolewa.