Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za kiafrika zatakiwa kubuni ajira za kisasa kwa muda wa miaka kumi inayokuja

Nchi za kiafrika zatakiwa kubuni ajira za kisasa kwa muda wa miaka kumi inayokuja

Shirika la kazi duniani ILO linataka kuchukuliwa hatua za dharura za kubuni nafasi milioni 600 za ajira kwa muda wa miaka kumi ijayo. ILO inasema kuwa ajira inahitajika ili kuwepo kwa maendeleo na uwiano wa kijamii. Kulingana na ripoti yake mpya ILO inasema kuwa bara la Afrika limekuwa na ukuaji mkubwa wa kiuchumi kwa miaka mingi iliyopita baada ya kujikuamua kutoka kwa hali ngumu ya uchumi.

Theo Sparreboom wa ILO amemuambia Patrick Maigua ya Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa tatizo lililoko kwenye ajira barani Afrika ni aina ya ajira ambazo zinapatikana.

(SAUTI YA THEO SPARREBOOM)