UNHCR yalaani mashambulizi kwa wakimbizi Sudan Kusini

UNHCR yalaani mashambulizi kwa wakimbizi Sudan Kusini

Takriban watoto 14 wakimbizi hawajulikani waliko na mmoja amejeruhiwa baada ya kuendeshwa kwa shambulizi la anga nchini Sudan kusini hiyo Jumatatu. Shambulizi hilo la anga lilifanyika katika eneo la Elfoj lililo kwenye jimbo la Blue Nile nchini Sudan Kusini.

Shambulizi hilo lilifanyika huku mabomu kadha yakidondoshwa kwenye kituo cha kupitishia wakimbizi kilicho karibu kilomita 10 kutoka kwenye mpaka na Sudan. Bomu la kwanza lilianguka wakati Kundi kutoka kwa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM lilikuwa likiongoza oparesheni za kuhamisha watu ambapo wakimbizi waliruka kutoka kwa malori na kutawanyika.Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)