WFP yashirikiana na makampuni kuziandaa nchi kukabiliana na majanga

WFP yashirikiana na makampuni kuziandaa nchi kukabiliana na majanga

Mashirika ya misaada ya kibinadamu na makampuni makubwa ya kiufundi duniani wameungana ili kufanya tathimini ya kwanza miongoni mwa nyingi za kuzisaidia nchi kuuimarisha uwezo wake wa kukabiliana na majanga ya dharura.

Makampuni ya A.P Moller-Maersk na UPS yamejiunga na makampni mengine yanayoongozwa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kufanya tathimini Nigeria, tathimini inayojikita katika uwezekano wa kuzuka majanga ya asili na mlipuko wa maradhi. Tathimini hiyo inaangalia viwango vya miundombinu kama barabara, madaraja, bandari na viwanja vya ndege. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)