Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO kutoa ripoti kuhusu hali na matatizo ya ajira duniani

ILO kutoa ripoti kuhusu hali na matatizo ya ajira duniani

Shirika la kazi duniani ILO Jumatatu jioni linatoa ripoti ya kila mwaka ya mtazamo wa ajira duniani. Ripoti hiyo inatoka wakati kukiwa na matatizo makubwa ya ajira na matarajio ya kuzorota zaidi hali ya uchumi duniani.

Ripoti hiyo iitwayo “Mtazamo wa kimataifa wa ajira 2012, kuzuia zaidi matatizo ya ukosefu wa ajira “ inatoa taarifa mpya za kimataifa na kikanda na matarajio katika viashiria mbalimbali vya soko la kazi duniani ikiwemo ajira, ukosef wa ajira, umasikini wa kazi na ajira mbaya.

Pia itawasilisha idadi ya sera za kuzingatiwa kutokana na changamoto mpya zinazowakapili watunga sera katika miaka ijayo kuhusu soko la ajira.