Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa misaada kwenye jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini

UM watoa misaada kwenye jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini

Mashirika ya Umoja wa Mataifa kupitia usaidizi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS yamezindua oparesheni kubwa ya kibinadamu kwenye mkoa wa Jonglei nchini Sudan Kusini ili kutoa usaidizi kwa jamii zilizoathiriwa na mizozo ya hivi majuzi.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa ghasia zilizoshuhudiwa zimesababisha kuhama kwa watu wengi. Lisa Grande afisa kwenye shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA akizungumza na Donn Bobb wa Radio ya ya UM amesema kuwa serikali ya Sudan imetangaza jimbo la Jonglei kuwa eneo la janga.

(SAUTI YA LISA GRANDE)