UNAIDS yazindua mradi wa kuwaunganisha vijana kupitia mtandao

5 Januari 2012

Shirika la kupambana na ugonjwa wa Ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS limezindua mradi kwa njia ya mtandao ulio na lengo la kuwaunganisha vijana. Mradi huo uliwaunganisha vijana kwa awamu mbili za kwanza kupitia kongamano nane kwa njia ya mtandao kwa lugha saba kote duniani ambapo vijana walijadiliana masuala muhimu yanayowahusu vijana na ugonjwa wa ukimwi.

Mradi huu ujulikanao kama CrowdOutAIDS umewaunganisha karibu vijana 20,000 kutoka karibu nchi zote duniani. Kwenye sehemu ambapo huduma za mtandao hazipatikani kuliandaliwa kongamano ili kuwafikia watu. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud