Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kubadilika kuambatana na karne ya ishirini na moja:Ban

Umoja wa Mataifa kubadilika kuambatana na karne ya ishirini na moja:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa Umoja wa Mataifa unastahili kufuata mabadiliko ya karne ya ishirini na moja ili uweze kukabiliana vilivyo na changamoto za dunia. Ban anaanza awamu yake ya pili kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi huu baada ya kuchanguliwa bila kupingwa mwezi Juni mwaka uliopita.

Amesema kuwa Umoja wa Maataifa utakabiliwa na changamoto kadhaa likiwemo suala la mabadiliko ya hali ya hewa, haki za binadamu na kuwalinda raia kwenye mzozo.