Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumzia misukosuko ya kikabila Sudan Kusini

Ban azungumzia misukosuko ya kikabila Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea wasi wasi uliopo kutokana na kuendelea kuwepo misukosuko ya kikabila katika jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini ambapo watu kadhaa wameuawa huku ripoti zikisema kuwa kundi la vijana waliojihami kutoka jamii moja wanajiandaa kuvamia jamii nyingine.

Kwenye taarifa kupitia kwa msemaji wake Ban amezungumzia misukosuko iliyopo kati ya jamii ya Lou Nuer na Murle. Ban ametoa wito kwa viongozi wa pande hizo mbili kuachana na ghasia na kushirikiana na serikali katika kupata suluhu la kudumu. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)