Matukio ya mwaka wa 2011 katika Umoja wa Mataifa
Mwaka wa 2011 umekwa wa habari na matukio kemkem kwenye Umoja wa Mataifa yaliyoghubika dunia nzima kwa ujumla. Kwani mwaka huu dunia imemkaribisha mkaazi wa bilioni 7, katika ulimwengu wenye migogoro na changamoto nyingi. Mamilioni wakighubikwa na njaa, wengine wakitafuta uhuru wa kujieleza na maisha bora kwao na familia zao. Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hakusita kutoa ujumbe maalumu.
(SAUTI YA BAN KI-MOON)