Mafuriko yakatili maisha na kusababisha athari kubwa Tanzania

22 Disemba 2011

Mji mkuu wa Tanzania Dar es salaam uko katika hali ya wasiwasi kufuatia mafuriko yaliyoghubika maeneo mengi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa ya Tanzania mvua hizo kubwa zitaendelea kunyesha kwa muda na imewashauri watu wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kuhama haraka. Hadi sasa watu takribani 20 wamepoteza maisha na mamia ya watu kulazimika kuzihama nyumba zao, kukiwa na uharibifu wa mali na miundombinu pia.

Watu wengi wanaoishi mabondeni nyumba zao zimebomolewa kabisa na mafuriko hayo na sasa wanaishi katika vituo vya dharura wakipatiwa msaada na washirika mbalimbali kikiwemo chama cha msalaba mwekundu, na Umoja wa Mataifa.

Stella Vuzo ni afisa katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya habari na mawasiliano mjini Dar es salaam.

(SAUTI YA STELLA VUZO)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter