Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afghanistan na mataifa jirani yashirikiana kupiga vita madawa ya kulevya

Afghanistan na mataifa jirani yashirikiana kupiga vita madawa ya kulevya

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayopambana na madawa ya kulevya pamoja na uhalifu UNODC imesema kuwa taifa la Afghanistan na mataifa ya Asia ya kati yamekubaliana kuzindua mpango wa miaka mitatu wa kupambana na mihadarati.

Uzinduzi huo unafanyika baada ya mkutano wa kimataifa ulioandaliwa mjini Bonn Ujerumani kuhusu siku za baadaye za Afhanistan wakati watakapoondoka wanajeshi wa kigeni mwaka 2014.

Inakadiriwa kuwa watu 100,000 wanaaga duniani kila mwaka kutokana na madawa ya kulevya yanayotengezwa na kutumiwa nchini Afghanistan. Mkurugenzi wa UNODC Yuri Fedotov anasema kuwa madawa ya kulevya yamekuwa tatizo kubwa katika eneo hilo.

(SAUTI YA YURI FEDOTOV)