Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matarajio ya mazunguzo kwenye mkutano wa Durban ni ya chini:Ban

Matarajio ya mazunguzo kwenye mkutano wa Durban ni ya chini:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amesema kwamba matarajio kwenye majadilioni kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa mjini Durban ni ya chini. Ban ameyasema hayo hii leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa majuma mawili kuhusu hali ya hewa ambapo mataifa yatakubaliana kuhusu kupunguza hewa chafu ili kuzuia kupanda kwa nyuzi ya joto duniani.

Mkutano huu pia utazindua mazungumzo kuhusu mfuko wa hali ya hewa wa kusaidia nchi maskini kuishi kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuzisaidia maskini kwenye matumizi ya teknolojia isiyochafua mazingira.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)