Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la mwisho la wahamiaji laelekea Ethiopia kutoka Tanzania

Kundi la mwisho la wahamiaji laelekea Ethiopia kutoka Tanzania

Kundi la mwisho la wahamiaji 150 kutoka Ethiopia ambao wamekaa kwenye magereza ya Tanzania kwa zaidi ya mwaka mmoja kama wahamiaji na waliokuwa na nia ya kurudi nyumbani wamesaidiwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kurejea mwakwao. Kundi hilo ni kati ya waethiopia 910 ambao wamesaidiwa na IOM mwaka huu.

Kabla ya kuondoka wahamiaji hao walipokea huduma za matibabu kutoka kwa wafanyikazi wa IOM ambapo wengi wao walipatikana kuugua ugonjwa wa Malaria na magonjwa mengine ya ngozi lakini hata hivyo walikuwa salama kusafiri ambapo pia IOM iliwapa kila mmoja nguo na viatu.

Mmoja wa wahamiaji hao aliiambia IOM kwamba baada ya kuwasili nchini msumbiji walilazimishwa kuvuka kwa kupiga mbizi mto Ruvuma ambao ni mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji. Jumbe Omari Jumbe wa IOM amezungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu suala hili

CLIP