Skip to main content

WFP na Konami wazindua mchezo kwenye mtandao wa kupambana na njaa

WFP na Konami wazindua mchezo kwenye mtandao wa kupambana na njaa

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwa ushirikiano na kampuni ya burudani ya Konami Digital Ltd ambayo inaongoza duniani kwa vifaa vya elektroniki wanazindua mchezo kwenye mtandao ambao utasaidia kuhusu masuala ya chakula Japan na kwingineko.

Kwa Mujibu wa mkurugenzi wa mawasiliano, sera na ushirikiano wa WFP Nancy Roman mchezo huo uitwao Food Force utawaweka wachezaji katikati ya shirika kubwa la misaada ya kibinadamu kuwa msitari wa mbele katika vita dhidi ya njaa. Na ili kusonga mbele wachezaji lazima wapate chakula, wakisambaze duniani na kukabiliana na hali za dharura wakati wakiendelea kulimbikiza msaada. George Njogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)