Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama limeongeza muda wa vikwazo vya silaha DRC

Baraza la Usalama limeongeza muda wa vikwazo vya silaha DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuongeza kwa mwaka mmoja zaidi vikwazo vya silaha na vikwazo vingine ilivyoviweka karibu miaka kumi iliyopita dhidi ya makundi ya wanamgambo wenye silaha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika azimio lililopitishwa bila kupingwa na wajumbe wote 15 wa Baraza la Usalama vikwazo vimeongezwa muda hadi tarehe 30 Novemba 2012 na limemuomba Katibu Mkuu kuongeza muda wa kundi na wataalamu wanaofuatilia hatua hizi na kuteua mtaalamu mwingine wa sita kwa ajili ya kufuatilia mali asili ya taifa hilo kubwa barani Afrika. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)