Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC yapongeza juhudi za kudhibiti madawa ya kulevya Afghanistan

UNODC yapongeza juhudi za kudhibiti madawa ya kulevya Afghanistan

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia dhidi ya madawa ya kulevya na uhalifu UNODC imepongeza makubaliano yaliyofikiwa baina ya mawaziri wa nchi za Pakistan, Afghanistan na Iran ambao wameweka shabaya ya pamoja na kukabiliana usambazwaji wa madawa hayo.

Mawaziri hao wote kwa pamoja wamefikia makubaliano ya kuongeza mashirikiano ya ubadilishanaji wa taarifa ili kudhibiti miendendo ya usambazaji na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Eneo hilo linakabiliwa na ongezeko la madawa ya kulevya huku Afghanistan pekee ikitajwa kusafirisha duniani kiasi cha asilimia 90 ya madawa ya kulevya aina ya kasumba.

Akitoa pongezi zake kwa mawaziri hao, Mkurugenzi Mtendaji wa ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa Yury Fedotov amesema kuwa hatua hiyo inatuma ishara njema namna pande hizo zilivyoweka shabaya ya pamoja kukabili changamoto ya ongezeko la madawa ya kulevya.