Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uharibifu na upungufu wa ardhi na maji ni tishio kwa usalama wa chakula:FAO

Uharibifu na upungufu wa ardhi na maji ni tishio kwa usalama wa chakula:FAO

Kuenea kwa mmomonyoko wa ardhi na upungufu wa ardhi na maji umeiweka mifumo mingi muhimu ya uzalishaji wa chakula duniani katika hatari na kutoa changamoto ya kuilisha dunia inayotarajiwa kuwa na watu bilioni 9 ifikapo 2050. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO na iliyochapishwa Jumatatu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo hali ya ardhi na rasilimaji ya maji duniani inatia mashaka hivi sasa ukizingatia kwamba miaka 50 iliyopita watu wameshuhudia ongezeko la uzalishaji wa chakula, lakini kwa sasa kwenye maeneo mengi mmomonyoko wa ardhi na upungufu wa ardhi hiyo na maji vimeweka usalama wa chakula njia panda baada ya kuathiri mifumo mingi ya uzalishaji. Jaques Diof ni mkurugenzi mkuu wa FAO.

(SAUTI YA JAQUES DIOF)