Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la kwanza la wakimbizi warejea nyumbani nchini Ivory Coast

Kundi la kwanza la wakimbizi warejea nyumbani nchini Ivory Coast

Mamia ya wakimbizi ambao walihama makwao kutoka na mzozo wa uchaguzi ulioikumba Ivory Coast wameanza kurejea nyumbani kwa usaidizi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Kundi la kwanza la watu 459 waliondoka kwenye kituo cha kimishenari cha Duekoue huku wengine wakitarajiwa kurejea makwao siku chache zijazo. Kwa sasa inakadiriwa kuwa watu 17,000 wanaishi kwenye kambi kote nchini Ivory Coast kando na maelfu ya wengine wanaoishi na familia zingine. Kuimarika kwa usalama kumewafanya wakimbizi wengi kurejea kwao vijijini. Jumbe Omari Jmbe afisa wa IOM anafafanua

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)