Kitabu kipya chaangazia umuhimu wa mali asili katika kuleta amani

15 Novemba 2011

Umuhimu wa siasa katika ujenzi wa idara za serikali, kuwepo uwajibikaji, juhudi za kupambana na ufisadi , usimamizi wa mali ghafi ili kuzuia mizozo ambayo inaweza kuleta vita ni kati ya masuala yaliyozungumziwa kwenye kitabu kinachozungumzia uwekaji amani baada ya mizozo na usimamizi wa mali asili.

Taasisi ya sheria kuhusu mazingira ELI,  Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na chuo kikuu cha Tokyo hii leo wametangaza kuchapishwa cha kitabu chao cha kwanza kuhusu uwekaji amani baada ya mizozo na usimamizi wa mali asili.

Kitabu hiki kinaangazia changamoto zinazokumba mataifa ambayo awali yamekumbwa na mizozo katika utumizi wa mali asili kwa ukuaji wa uchumi , kwa mapatano na ajira bila ya kuwepo uharibifu wa mazingira.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter