Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila mmoja ana jukumu la kuwalinda raia katika maeneo ya vita:Ban

Kila mmoja ana jukumu la kuwalinda raia katika maeneo ya vita:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni jukumu la kila mtu kufanya juhudi kuwalinda raia wanaojikuta katikati ya migogoro ya vita. Akizungumza katika mjadala wa Baraza la Usalama Jumatano uliokuwa ukizungumza haja ya kuwalinda raia katika maeneo ya vita Ban amesema vita vinapozuka duniani kote wanawake, wasichana, wavulana na wanaume wanaendelea kubeba mzigo wa vita hivyo na mara nyingi haki zao za binadamu zinakiukwa ikiwa ni pamoja na sheria za kimataifa. Ameongeza kuwa ukiukwaji huo ni pamoja na mauaji, utesaji, utekwaji, ubakaji na ukatili.

Amesema pia dunia hushuhudia watu wakishinikizwa kuingia jeshini kupigana wakiwemo watoto, ambao wengi hawapati huduma za afya na msaada wa kuokoa maisha yao, pia watu wengi hutawanya na vita hivyo na wanaishia kwa tegemezi na kupoteza fursa nyingi katika maisha yao. Ametaka kila mmoja kukumbuka kwamba watu hawa wanateseka kwa sababu ya maksudi ya  watu wengine.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)