Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu wakimbizi na wahamiaji waandaliwa Djibouti

Mkutano kuhusu wakimbizi na wahamiaji waandaliwa Djibouti

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ni kati ya wanaohudhuria mkutano uliondaliwa na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na serikali ya Djibout unaojadili njia za kushughulikia wahamiaji na wanaofatafuta hifadhi wakati wanapojipata kwenye shida baharini.

Mkutano huo unaongo’a nanga hii leo mjini Djibouti unawaleta pamoja waakilishi wa serikali na wasomi wakiwemo wataalamu kutoka UNHCR, IOM, Chama cha mabaharia miongoni mwa wengine.

Suala la kuhama kwa raia wa Somalia na Ethiopia kupitia Ghuba ya Aden limekuwa likiangaziwa ikiwemo idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili nchini Australia pamoja na wahamiaji kutoka Kaskazini mwa Afrika wanaoingia barani Ulaya. Jean-Philippe Chauzy ni msemaji wa IOM, lakini nitakujulisha

(SAUTI YA JEAN-PHILLIPPE CHAUZY)