Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi waandaliwa nchini Liberia huku UM ukitaka kuwepo kwa amani

Uchaguzi waandaliwa nchini Liberia huku UM ukitaka kuwepo kwa amani

Kulishuhudiwa hali ya wasi wasi kwenye mji mkuu wa Liberia hii leo huku kukiwa na milolongo mirefu ya wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura hata baada ya wito wa upinzani wa kutaka kususiwa kwa uchaguzi huo.

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia Ellen Margaret Loj anasema kuwa kupiga kura ni uamuzi wa mtu akiongeza kuwa Mliberia yeyote aliye na nia ya kutekeleza haki yake ana haki ya kufanya hivyo kwa amani na bila kukandamizwa.

(SAUTI YA MARGARET LOL)

Loj amewataka waliberia kukataa ghasia na wasaidie kuijenga nchi yao kidemokrasia.