Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua kubwa yazua madhara zaidi kwa wakimbizi wa Kisomalia

Mvua kubwa yazua madhara zaidi kwa wakimbizi wa Kisomalia

 

Maelfu ya Wasomali waliohama makwao kwa sasa wameathiriwa na mvua kubwa pamoja na mafuriko yanayoshuhudiwa nchini Somalia, Kenya na Ethiopia.

Kumeshuhudiwa mafuriko kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo makao ya karibu watu 2800 kwenye kampi ya Sigale yamefurika. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesambaza misaada kwa weaathiriwa huku misaada zaidi inatarajiwa kusambazwa kwenda sehemu zilizoathirika zaidi na kambi za wakimbizi. Andrej Mahecici ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)