Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha mchango wa wahandisi kutoka Japan

Ban akaribisha mchango wa wahandisi kutoka Japan

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha uamuzi wa kuchangia waandisi kwenye kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilicho Sudan Kusini cha UNMISS. Ban amesema kuwa waandisi hao watachangia kwenye jitihada za kuisaidia serikali kujenga baadhi ya miundo mbinu . Kulingana na msemaji wa Ban ni kuwa kampuni ya uandisi kutoka Japan inatarajiwa kuungana na kikosi cha Umoja wa Mataifa kilicho Sudan Kusini UNMISS Januari mwakani. UNMISS kwa sasa ina wanajeshi 5600 nchini Sudan Kusini.