Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zitumie haki kwenye manunuzi ya vyakula ili kuinua wakulima wadogo: mtaalamu

UN Photo/Marco Dormino
UN Photo/Marco Dormino

Serikali zitumie haki kwenye manunuzi ya vyakula ili kuinua wakulima wadogo: mtaalamu

Manunuzi ya vyakula vya umma yanayofanywa na serikali ni lazima yalenge kuinua wazabuni na wakulima wadogo wadogo ingawa kwamba hatua hiyo awali huwa ni gharama kubwa.

Amesema mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula Olivier De Schutter siku ya Alhamisi akieleza kuwa kwenye mfumo wa manunuzi ya chakula duniani uliokubwa na utandawazi misingi mitano inapaswa kuzingatiwa ili kuhakikisha haki ya chakula inatimizwa.

Ripoti ya De Schutter inataka serikali zinaponunua vyakula kwa ajili ya taasisi za umma kama vile hospitali na shule kuzingatia misingi hiyo ambayo ni pamoja na kununua kutoka kwa wazalishaji wadogo na kuwawezesha kupata zabuni.

Amesema ni gharama kubwa kununua kutoka kwa wazalishaji au wasambazaji wadogo lakini baada ya muda mrefu inajenga uwezo kwa wakulima kwani bidhaa zao zinakuwa zina uhakika wa soko.

Msingi mwingine ni kuweka hakikisho la mishahara na bei sawia kwenye mifumo ya usambazaji wa vyakula na kuweka masharti maalum ya kuwezesha upatikanaji wa milo kamili.

Mtaalamu huyo amepongeza Brazil ambako hivi sasa kumewekwa utaratibu kuhakikisha asilimia 30 ya manunuzi ya vyakula vya shule yanatoka mashamba ya familia.