Vijana barani Afrika wanasema wakati umefika wa kusikilizwa

28 Oktoba 2011

Kila mwaka Novemba mosi vijana kote barani Afrika wanaadhimisha siku yao kwa hafla na shughuli mbalimbali ikiwemo mijadala na maandamano.

 Mwaka huu kimataifa siku hii inaadhimishwa nchini Afrika ya Kusini ambako vijana kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika watakutana kuanzia Novemba mosi na pili Gauteng mjini Johanesburg.

Mbali ya maadhimisho vijana hao watajadili pia matatizo yanayowakabili vijana, kupendekeza suluhisho, kubadilishana mawazo na kutafuta njia za kuimarisha muungano miongoni mwa vijana barani Afrika.

Ili kujadili umuhimu wa siku hii kwa vijana, yapi yanayowatatiza na nini mapendekezo yao, Flora Nducha ameketi na baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Kimarekani USIU kilichopo mjini Nairobi nchini Kenya  na kujadili nao.

(MJADALA NA WANAFUNZI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud