Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma bora za hali ya hewa zitakabiliana na ukame:WMO

Huduma bora za hali ya hewa zitakabiliana na ukame:WMO

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO limesema kuwa maendeleo ya kisayansi yameweka msingi bora wa sera za kukabiliana na kiangazi na kuenea kwa majangwa. Usalama wa chakula na maji ni kati ya sehemu zitakazoshughulikiwa kwenye mpango wa hali ya hewa wa WMO na washirika wake. Mpango huo una lengo la kuhakikisha kuwepo kwa habari kuhusu hali ya hewa kwa wakati ufaao kwa nchi zote hasa zinazoathirika zaidi. Mkurugenzi wa WMO Michel Jarraud anasema kuwa mpango huo mpya kuhusu huduma za hali ya hewa kitakuwa kifaa muhimu cha kukabiliana na ukame na kuongezeka kwa majangwa. Claire Nullis ni msemaji wa WMO.

(SAUTI YA CLAIRE NULLIS)