Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ta kutokomeza Umaskini

Siku ya kimataifa ta kutokomeza Umaskini

Zaidi ya watu bilioni moja duniani ni masikini na wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku, hali ambayo imetiwa mkazo leo katika siku ya kimataifa ya kutokomeza umasikini.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “kutoka katika umasikini kuelekea maisha bora:watu ndio kitovu cha maendeleo kwa wote”.  Akitoa ujumbe maalumu kuhusu siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kwa miongo kadhaa Umoja wa Mataifa umekuwa ukijitahidi kuwasaidia watu kutoka kwenye dimbwi la umasikini lakini haitoshi.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Tangu mwaka 1957 shirika lisilo la kiserikali liitwalo Atd Fourth World limekuwa likifanya kazi katika nchi zote duniani kuelimisha kuhusu umasikini na jinsi gani ya kuwatoa watu katika mzunguko huo. Mwakilishi wa shirika hilo Geneva ni Janet Nelson.

(SAUTI YA JANET NELSON)