Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yatakiwa kuwahakikishia watoto lishe bora

Mataifa yatakiwa kuwahakikishia watoto lishe bora

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linatarajiwa kuyaunganisha maisha ya watoto kutoka nchi zinazoendelea duniani wanaoishi kwa njaa kwa wahisani wanaoweza kuwasaidia wakati wa maadhamisho ya siku ya chakula duniani.

Mkurugenzi mkuu wa WFP Jesette Sheeran anasema kuwa chakula kizuri ndiyo nguzo ya kukua kwa mtoto aliye na afya akiongeza kuwa huu ndio wakati wa kumaliza njaa na utapiamlo. Wakati wa maadhimisho haya naye katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amewashauri viongozi kwenye nchi tajiri sawia na nchi maskini kuwekeza kwenye miradi ambayo itasaidia kumaliza njaa ikiwa ndiyo nguzo ya kuafikia malengo ya maendeleo ya milenia.