Ugaidi na uhusiano wake na uhalifu uliopangwa

Ugaidi na uhusiano wake na uhalifu uliopangwa

Kamati ya Umoja wa Mataifa iliyotwikwa jukumu la kusaidia nchi katika kukabiliana na ugaidi hii leo imeelezea uhusiano uliopo kati ya ugaidi na uhalifu uliopangwa ukiwemo usafirishaji haramu wa silaha hatari za nyuklia, kemikali, baolojia na bidhaa zingine hatari.

Kwenye mkutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Kamati hiyo iliyobuniwa baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mjini Newyork ilisisitiza kuwa hata kama kumekuwa na mafanikio kwa muda wa miaka 10 iliyopita bado mengi yanasalia kufanyika katika ngazi za kitaifa na kimataifa. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)