Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muungano wa Afrika na UM waafikiana kuimarisha ushirikiano kuchagiza amani

Muungano wa Afrika na UM waafikiana kuimarisha ushirikiano kuchagiza amani

Viongozi wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika wameafikiana kuanzisha juhudi za pamoja kukabiliana na baadhi ya migogoro mikubwa na masuala ya usalama barani Afrika. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika Jean Ping kwenye mkutano wao umejikita katika ushirikiano uliopo baina ya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika, na maendeleo ya matukio mbalimbali ikiwemo suala la Libya, Somalia, Sudan na Sudan Kusini.

Tangu mwaka 2008 mashirika hayo mawili yamekuwa yakifanya kazi za kulinda amani pamoja hasa kupitia mpango wa kulinda amani Darfur ujulikanao kama UNAMID, na Somalia vikosi vya kulinda amani vya muungano wa Afrika AMISOM vinasaidia na Umoja wa Mataifa.